ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka. Ukishaguswa na muziki huo sio ajabu ukajiuliza swali gumu; kwanini mungu akamchukua Mbaraka Mwaruka Mwinshehe baada ya ile ajali ya gari nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979? Angelikuwa hai nani asingependa kusoma mahojiano yake? Inasemekana Mbaraka Mwinshehe alikufa kutokana na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake. Alifia hospitalini Mombasa.






Uwezo wake wa kutunga nyimbo, kupanga muziki na kudonoa gitaa hauna mfano wake mpaka sasa. Ukimsikiliza leo unaweza dhani kapiga gitaa hilo juzi kumbe ni miaka chungu mbovu iliyopita. Kizuri zaidi ni kwamba upigaji wa gitaa hakufundishwa na mtu bali yeye mwenyewe. Akiwa bado kijana mdogo kabisa alicheza muziki uliokuwa unajulikana kwa jina la “kwela”(asili yake Afrika Kusini) na bendi iliyojulikana kama Cuban Branch Jazz.




Mbaraka alianza kujitengenezea jina kwenye medani ya muziki wakati alipokuwa mmojawapo ya wanamuziki waliokuwa wanaunda bendi maarufu ya Morogoro Jazz kati ya mwaka 1964 mpaka 1973. Baadaye ndipo alipoanzisha bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Super Volcano mwaka 1973. Alidumu na kutamba na Super Volcano mpaka mauti ilipomfika miaka sita baadaye. Kuimba alijifunza kutoka kwa Salum Abdullah, mwanzilishi wa Morogoro Jazz ambaye baadaye alijiengua na kwenda kuunda Cuban Marimba Band.
Hii hapa ni baadhi tu ya miziki ya Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ambayo inatufanya tuendelee kumkumbuka daima. Lala pema peponi


Huwezi Amini Mtu Huyu Kuongoza America


Huwezi jaribu fikiria ila yote yanawezekana chini ya jua kila kitu kinawezekana.

Nakaaya na hatua za juu zaidi


Inakua hatua ya juu zaidi pindi unapo hojiwa na kituo cha maghalibi kama bbc ama cnn sasa huyu dada yetu mpendwa ameweza kufika huko na kuhojiwa katika kipindi cha cnn inside Africa tumeipenda hiyo.

Peter out


Peter katoka nje ya maisha plus lakini hata hivyo kala bingo tbc kwa ajili ya sauti yake kuvutiwa na wakubwa wa tbc hongera imekua njia ya kutokea brother big up.

Bodi ya Tanesco inasubiri nini kujiuzulu?


Bodi ya Tanesco inasubiri nini kujiuzulu?

Ni jambo la kufedhehesha kwamba eti Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk. Idirs Rashid, amekiuka maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo juu ya mitambo ya kufua umeme ya Dowans.

Kwamba bodi ikiwa na akili timamu kabisa iliagiza menejimenti ya shirika hilo kwamba iachane na mitambo ya Dowans, lakini Dk. Rashid akapuuza maelekezo hayo na kwenda kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kuwasilisha kilio cha kutaka kuinunua kutokana na kilichoelezwa uhaba wa umeme utakaokabili taifa baadaye mwaka huu.

Baada ya Dk. Rashid kuwasilisha hoja yake kwa Kamati hiyo, amekutana na upinzani mkali kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya nia ya Tanesco ya kununua mitambo hiyo.

Lakini zaidi kauli ya bosi huyo aliyotoa mbele ya waandishi wa habari wakati akitangaza kwamba wameondoa nia yao ya kuwania kununua mitambo hiyo, nayo imeudhi watu wengi kutokana na kutishia wananchi kwamba taifa litaingia gizani na wasilaumiwe.

Kwa ujumla suala la mitambo ya Dowans limefunikwa na sintajua nyingi, ukiukaji wa taratibu na upuuzaji wa maelekezo kwa upande wa watendaji wa Tanesco kiasi cha kuamsha maswali mengi na magumu juu ya sababu ya hali hiyo kutokea.

Yapo maelezo mengi yametolewa juu ya mitambo ya Dowans wapo wanaosema kwamba mitambo hii ni muhimu kwa ajili ya kufanikisha mikakati ya Tanesco kujipanga kukabiliana na uhaba wa maji katika mabwawa pia wapo wanaosema kwamba mitambo hiyo ikinunuliwa itapunguza adha na mchakato mrefu wa kuanza kuagiza mitambo mipya.

Pamoja na misimamo ya hoja hizo hapo juu, wapo wanaosema kwamba mitambo ya Dowans ni haramu kutokana na kuwa na mahusiano na mkataba wa kampuni ya Richmond Development Corporation iliyoingia mkataba wa kilaghai na Tanesco mwaka 2006.

Kwa kuzingatia hali hiyo pamoja na azimio la Bunge juu ya mkataba wa Richmond, pengine ndiyo maana Bodi ya Tanesco ikijua utata uliogubika mchakato wa mkataba huo, ilijiepusha na mipango ya kutaka kuinunua Dowans kwa sababu ya vikwazo vya kisheria.

La kushangaza ni kwamba eti bodi baada ya kutoa maelekezo yake kwa menejimenti ya Tanesco ambayo yamepuuzwa, inafanya kampeni za chini chini ili muda wa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ukiisha baadaye mwaka huu, usiongezwe!

Yaani bodi imekwama kiasi kwamba haiwezi kumuwajibisha Mkurugenzi huyo au walau kuandikia mamlaka ya uteuzi wake kwamba kiongozi huyo amekiuka maelekezo yao na kwa maana hiyo aondolewe.

Bodi ya Tanesco imekuwa kama boya tu, haina nguvu wala uwezo wa kumfanya lolote Mkurugenzi Mtendaji hata pale anapoipuuza wazi wazi.

Tunajiuliza hivi Bodi ya Tanesco ina nguvu gani basi kwa ajili ya uendeshaji wa shirika hili pekee la kuzalisha nishati ya umeme nchini?

Kama Bodi haiwezi hata kumkemea Mkurugenzi Mtendaji hata pale anapoipuuza, ina sababu gani basi ya kuendelea kuwapo madarakani? Inalinda maslahi ya nani?

Sisi tunafikiri Bodi ya Tanesco kama imeshindwa kukata pembe za Dk. Rashid ina moja tu la kufanya, kujiuzulu mara moja kama ishara ya kulinda heshima yao, lakini la pili, kuwasilisha ujumbe kwa umma kwamba hawakubaliani na vitendo vya kuvunjwa kwa sheria kanuni na taratibu.

Kama Bodi haitaki kujiuzulu, ni lazima wahakikishe Dk. Rashid anajiuzulu mwenyewe ili kulinda heshima yao.

Kama haya hayatatokea, tunashawishika kusema Bodi hii haina kazi Tanesco na ni vema tu ikajiondoa yenyewe.

  • SOURCE: Nipashe

Ubinafsi wa P Funk waiangusha Bongo Records


Producer aliyekua maarufu lakini anaonekana kupotea kwa kutaka kupeleka studio yake kifamilia zaidi kuliko kibiashara sasa inaelekea kumtokea puani wakati nyimbo zake zinapotupwa kapuni kutokana na kushuka kiwango uwezo wake huku akimuacha Master J na Mj Records yake ikiwa juu vibaya kwa kujaribu kushirikiana na producers wengine kama macochali na wengine aliyo wahi kufanya nao kazi.

Wema Sepetu Miss tz 2006 Kizimbani




MISS Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu na mwenzake, Asha Jumbe, wakazi wa Tabata Senene jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na tuhuma ya kuharibu mali.

Akisoma hati ya shtaka hilo, Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwahy mbele ya Hakimu Mfawidhi Emillius Mchauru alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 29 majira ya saa 3:00 usiku maeneo ya Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.

Nassoro alidai kuwa siku ya tukio hilo watuhumiwa hao waliharibu kioo cha mbele cha gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba ya usajili T.993 ASD.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kioo cha gari kina thamani ya Sh 1,000,000 mali ya Stephen Kanumba.

Hata hivyo, watuhumiwa hao walikana shtaka hilo na walipelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya Sh 500,000, wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikalini.

Awali, mtuhumiwa wa kwanza alikuwa ana mdhamini, lakini cha kushangaza alipofika mahakamani hapo alidai kuwa alikuwa amesahau barua zake kwenye gari.

"Mheshimiwa hakimu naomba nikachukue barua za kumdhamini kwani nimezisahau kwenye gari nilipoitwa mimi nikaja bila kuzichukua, "alisema mdhamini wa mtuhumiwa wa kwanza

Baada ya muda kupita hakimu Mchauru alisema, "Yaani mahakama imsubiri mtu aenda nyumbani kuchukua barua za kumdhamini mtu, kesi hii naiahirisha hadi hapo itakapotajwa tena Machi 18".

Vifo na mateso ya wana apolo toka kwa wawekezaji


Tumesikia kesi nyingi toka migodini kuwa wana apolo huwa wanafanyiwa vitendo vya kinyama hadi wengine kufikia kupoteza uhai yote ni serikali kutopanga mikakati madhubuti kwa wananchi wake wa hali ya chini ambao ndio wapiga kula wengi na wanaoiweka serikali madarakani wakiwa na imani matatizo yao yata tatuliwa kwa wakati lakini iko tofauikabisa kwao hadi kufikia kukata tamaa.

Kushuka asilimia kumi ya kufaulu liwapi tatizi




Wanafunzi walio fanya mtihani wa kidato cha nne wmaka 2008 wamefeli kwa asilimia kumi zaidi kuliko miaka mingine iliyopita sasa sijui serikali inafanya jitihada gani ya kuokoa hili tatizo kwani wanafunzi wamesha kata tamaa ya kusoma kwa kutumia akili zao na kusubiria kupokea feki toka kwa wazazi wanaofanya kazi wizarani hivyo ni tatizo kubwa kwa taifa letu.

Mialiko ya wasanii ikulu iko wapi faida yake

Mialiko mingi tuliyosikia mkuu wa nchi kuwa alika wasanii tokea kipindi walicho jitolea kumfanyia kampeni ili kuingia madarakani kwa kula nyingi mwaka 2005 zili toka ahadi nyingi za kuwasaidia wasanii lakini nyingi zimekua hazitekelezeki hadi wasanii wanakata tamaa mara kadhaa wamekua wakialikwa lakini sijui wanakua na uwoga wa kuulizia ahadi zao walizo haidi ukaribu wao na ikulu umeathiri hata wasanii wa hiphop kushindwa kuzungumzia matatizo yanayo wagusa wananchi mfano ufisadi wanakalia kusifia machache mazuri yaliyofanywa huku asilimia nyingi ya mashabiki na raia walio tegemea kuona wasanii wanainua sauti zao kukemea wameywea kama maji.

Wasanii wa bongo na kujisahau


Wasanii wa kibongo huwa wanafeli kufikia malengo yao kwa sababu ya starehe zilizo pitiliza na kujikuta baada ya muda wanakua wamechoka vibaya na kurudi maisha ya ufukara kama zamani walivyokua tumeshaona mifano ya wsanii kibao waliyo fanikiwa na sasa wameanguka hawajiwezi.

Kujinyonga si suluhisho

Wiki mbili za hivi kaburini vyombo vingi vya habari vimetangaza habari za watu walio jinyonga bila ya kuacha taarifa kamili za kujinyonga kwao ila wengi ya wale wanao bahatika kuacha habari zao inakua ni kwa ajili ya mapenzi au maisha kuwa magumu kwao lakini si suluhisho iweje ukatize maisha yako wakati badi kuna ndugu zako wana kutegemea.

Kujinyonga si suluhu


Wiki mbili hizi zilizopita kume patikana na taarifa nyingi za watu kujinyonga bila ya kuacha taarifa kamili za kutenda kitendo hicho lakini wengi waliowahi kuacha ujumbe huwa u

Albino kuitwa dili sio sahihi











Kama binadamu mwenye akili toimamu na una maadili ya kidini au ya kiroho tu basi utakubaliana kuwa unyama na ukatili wanao tendewa ndugu zetu albino unawaumiza na kuwatia hofu ya kuishi kwa amani sheria zinazo simamia makosa kama hayo sijaona kutenda kazi vizuri zaidi ya kuchelewesha hukumu huku ushahidi upo kila kona serikali angalieni hili.

Mapenzi au Pesa na Rangi


Utakuta binti au mvulana mdogo ana anzisha uhusiano na bibi au babu wa kizungu na wanaweza wakafunga ndoa isiyo kua na baraka za wazazi au marafiki wa karibu wengi hufata rangi nyeupe na mambo ya mshiko na kusahau hisia zao za mapenzi zinahitaji nini angalieni sana wenye hii tabia ni htatari.

Ulaya au America na Vijana


Imekua kasumba siku hizi kila binti au mvulana anapenda maisha ya kuishi ughaibuni lakini hali huwa tofauti wafikapo huko kama mtu alikua si malaya basi atakua malaya au kama alikua si mlevi atakua mlevi yani kila starehe anakua anaijua yeye kwa sababu hakuna ndugu waa jamaa aliye karibu naye si tabia nzuri kwa kweli.

Liyumba na Mapesa ya watanzania


Aliyekua akiitwa Muheshimiwa sasa ni mtuhumiwa anahitaji kupata adhabu kubwa toka kea watanzania kwani ingekua China angepigwa risasi hadharani ila kwa kua bongo tuna mazoea ya wanao ongoza Tanzania wanakua mioyo yao imetawaliwa na imani za kidini lakini kiongozi bora ni yule anayekua na roho mbaya ndiyo maendeleo yatakuja kwa nchi.

Habari ya kwanza

Hellow washkaji life iko ngumu lakini si lazima kuaribu malengo yako kwa kukata tamaa jipe tumaini ubadili maisha.