ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka. Ukishaguswa na muziki huo sio ajabu ukajiuliza swali gumu; kwanini mungu akamchukua Mbaraka Mwaruka Mwinshehe baada ya ile ajali ya gari nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979? Angelikuwa hai nani asingependa kusoma mahojiano yake? Inasemekana Mbaraka Mwinshehe alikufa kutokana na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake. Alifia hospitalini Mombasa.






Uwezo wake wa kutunga nyimbo, kupanga muziki na kudonoa gitaa hauna mfano wake mpaka sasa. Ukimsikiliza leo unaweza dhani kapiga gitaa hilo juzi kumbe ni miaka chungu mbovu iliyopita. Kizuri zaidi ni kwamba upigaji wa gitaa hakufundishwa na mtu bali yeye mwenyewe. Akiwa bado kijana mdogo kabisa alicheza muziki uliokuwa unajulikana kwa jina la “kwela”(asili yake Afrika Kusini) na bendi iliyojulikana kama Cuban Branch Jazz.




Mbaraka alianza kujitengenezea jina kwenye medani ya muziki wakati alipokuwa mmojawapo ya wanamuziki waliokuwa wanaunda bendi maarufu ya Morogoro Jazz kati ya mwaka 1964 mpaka 1973. Baadaye ndipo alipoanzisha bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Super Volcano mwaka 1973. Alidumu na kutamba na Super Volcano mpaka mauti ilipomfika miaka sita baadaye. Kuimba alijifunza kutoka kwa Salum Abdullah, mwanzilishi wa Morogoro Jazz ambaye baadaye alijiengua na kwenda kuunda Cuban Marimba Band.
Hii hapa ni baadhi tu ya miziki ya Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ambayo inatufanya tuendelee kumkumbuka daima. Lala pema peponi


No comments: